MOHD TechnologiesMOHD TechnologiesIngiaNataka kuongea nanyi

Kwa shule, biashara na ofisi

Ukiondoka siku moja, kila kitu kinasimama?

Tunakusaidia kupata wateja wapya, kujibu kila mteja, kujua faida yako na kupata muda wako tena.

Pesa, watu na mafunzo yao, mahali pamoja: kila mtu anaona kazi yake, wewe unaona yote.

Unasafiri, unapumzika, na taasisi inaendelea bila wewe.

Maswali mawili, kisha tunakuonyesha kwenye simu yako.

  • Pesa yako inabaki yako: MOHD haishiki fedha za wateja.
  • Taarifa zako zinalindwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022.
  • Kila kitu kinawekwa kwenye akaunti zako mwenyewe.
  • Tunatumia sisi kwanza kila tunachokuwekea.

WanatuaminiMarashi Tree GardenFun Essence WorldOlmasai Legal & Labour SolutionsVivid Dream Schools

Nataka kusoma kwanza ↓

Huduma

Tunachotumia sisi, tunakuwekea na wewe

Kila huduma inaanza na kinachokusumbua leo, na inaishia na muda wako kurudi. Zote zinawekwa kwenye akaunti zako mwenyewe.

Tovuti

Wateja hawakupati mtandaoni?

Mteja anakutafuta mtandaoni, hakupati, anaenda kwa jirani yako.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Wateja wakupate mtandaoni

Akikutafuta anakupata, anaona unachofanya, na anakuandikia papo hapo.

Kesho: Wateja wapya wanakujia wenyewe, hata ukiwa umelala.

Tovuti hii, na tovuti za programu zetu, kila moja kwenye anwani yake.

Nataka tovuti inayoniletea wateja

Msaidizi wa WhatsApp

Wateja wanaandika usiku, nawe umelala?

Wateja wanaandika usiku na wikendi; ukijibu asubuhi wameshaenda kwa mwingine.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Kila mteja ajibiwe, hata usiku

Kila mteja anajibiwa papo hapo, kwa Kiswahili chako; swali gumu linakufikia wewe.

Kesho: Unazima simu jioni bila hofu ya kupoteza mteja.

Ukituandikia 0742 537 555, anayekujibu ni msaidizi wa aina hii.

Nataka kila mteja ajibiwe

App ya Play Store

Wateja wako hawana njia rahisi ya kukufikia kwenye simu?

Wateja wanataka kukufikia kwa simu, lakini kila kitu ni ujumbe uliotawanyika.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Jina lako kwenye simu ya mteja

Jina lako na nembo yako viko kwenye simu ya mteja; anafungua, anaona kilicho chake.

Kesho: Unakumbukwa kila siku, na wateja wanarudi bila kukumbushwa.

Maarifa, Mapato na Maslahi zinafungwa kwenye simu yoyote, hata bila mtandao.

Nataka app yangu mwenyewe

Publish

Unamsubiri fundi kila ukitaka kubadilisha tovuti yako?

Kila ukitaka kubadilisha bei au picha, unamsubiri fundi siku kadhaa.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Badilisha tovuti yako mwenyewe, kwa simu

Unaandika habari, tangazo au namba mpya kwenye simu, na tovuti inabadilika.

Kesho: Tovuti yako inaishi pamoja na biashara yako, bila kumtegemea mtu.

Habari na matangazo ya tovuti hii yanabadilishwa hivi, kutoka kwenye simu.

Nataka kubadilisha tovuti yangu mwenyewe

Mifumo inayojiendesha

Kazi zilezile za mkono zinakula siku yako?

Kila siku unafanya kazi zilezile kwa mkono: kunakili, kukumbusha, kutuma ripoti.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Saa zako zirudi

Kumbukumbu, ripoti na vikumbusho vinajituma vyenyewe kwa wakati.

Kesho: Saa zinazorudi unazitumia kukuza kazi yako, au kupumzika.

Tovuti hii inajikagua kila usiku; ikikuta kosa, inarudi ilivyokuwa yenyewe.

Nataka kazi zangu zijifanye zenyewe

MOHD Academy

Kila mfanyakazi mpya unamfundisha upya?

Kila mfanyakazi mpya unamfundisha upya, na hujui kama amejifunza kweli.

Tunafanya hivi ili kupunguza maumivu hayo:

Timu inayojua kazi yake

Kila mmoja anajifunza kwa simu yake, hatua fupi, na anapata cheti kinachohakikika mtandaoni.

Kesho: Unaweza kuondoka siku moja, na kazi inaendelea vizuri.

Timu yetu inajifunza hivyohivyo, kwenye MOHD Academy.

Nataka timu yangu ifundishwe

Nionyeshe huduma zote, kwa tatizo langu

Nini kinabadilika

Si programu tu. Ni uhuru wako unaorudi.

Muda wako, usingizi wako na amani ya moyo: hivyo ndivyo tunavyokurudishia.

  • JanaKila kitu kinakusubiri weweBei, mishahara, maamuzi: simu zinaita muda wote.
  • LeoKila mtu anajua kazi yakePesa, watu na mafunzo yao unaviona kwenye simu yako, kwa Kiswahili.
  • KeshoUnasafiri, unapumzikaTaasisi inaendelea, na unajenga kitu cha kurithisha.

Ni siku yako ipi kati ya hizi?

Ada zinaingia kila njia, na mwisho wa muhula hujui nani amelipa nini?

Sasa unaona leo nani amelipa na nani bado, na mzazi anaona deni lake mwenyewe.

Muda wako unarudi kwa watoto na walimu, na wazazi wanaiamini shule yako.

Nionyeshe Maarifa →

Unauza siku nzima, lakini jioni hujui faida iko wapi?

Sasa kila jioni unajua umeuza kiasi gani na nani bado hajakulipa, hata ukiwa mbali.

Unawaachia watu wako biashara, na unafungua tawi la pili kwa takwimu, si kwa kubahatisha.

Nionyeshe Mapato →

Je siku yako ya mshahara ni siku ya presha?

Sasa mishahara na makato yanahesabiwa kwa ajili yako, na tarehe za kulipa serikali ziko mbele yako.

Unakuwa mwajiri ambaye watu wanataka kumfanyia kazi.

Nionyeshe Maslahi →

Nionyeshe ya kwangu

Mfano wako, kabla hatujaanza

Andika jina la biashara yako. Tunachora papo hapo mwanzo wa tovuti yako, au salamu ya msaidizi wako wa WhatsApp, kama picha unayoweza kuhifadhi na kumtumia mtu.

Andika angalau herufi 2.

Hakuna kinachotumwa wala kuhifadhiwa: picha inachorwa kwenye simu yako.

Picha yako itaonekana hapa.

Jinsi tunavyofanya kazi

Hatua nne, bila mshangao

  1. 01

    Tunakusikiliza

    Unatuandikia WhatsApp. Tunakuuliza maswali mawili kuhusu kazi yako, kwa maneno yako.

  2. 02

    Tunakuonyesha

    Unaona inavyofanya kazi kwenye simu yako kabla ya kuamua. Bei inakuja baada ya kukusikiliza.

  3. 03

    Tunaweka

    Kila kitu kinawekwa kwenye akaunti zako mwenyewe, kwa jina lako, na kinakaguliwa kabla ya kuwa hewani.

  4. 04

    Tunafundisha

    Timu yako inajifunza kwa simu, hatua fupi, na inapata cheti. Kazi inaendelea bila wewe kuwepo kila saa.

Tunachokuwekea, tunakitumia sisi kwanza

Nionyeshe kazi mlizofanya

Kazi yetu, kwa ruhusa ya wenyewe

olmasai.co.tz
Olmasai Legal & Labour Solutionsolmasai.co.tz

Olmasai Legal & Labour Solutions

Ushauri wa sheria na kazi

Mwenye swali la kazi au sheria anawapata mtandaoni, anasoma huduma kwa lugha yake, na anawaandikia moja kwa moja.

Vivid Dream Schools
Vivid Dream Schools

Vivid Dream Schools

Shule, Zanzibar

Wazazi wapya wanaiona shule kwenye simu, maisha yake na jinsi ya kujiunga, na wanaandika moja kwa moja.

Kwa nini utuamini

Imani inajengwa kwa ukweli, si kwa maneno

Pesa yako inabaki yako

MOHD haishiki, haipokei wala haihamishi fedha za wateja wako. Malipo yanaenda moja kwa moja kwenye akaunti zako.

Taarifa zako zinaheshimiwa

Tunafuata Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Na. 11 ya 2022). Hatuuzi taarifa za mtu yeyote, wala hazitumiki kwa matangazo.

Nataka kusoma zaidi

Hakuna anayeshika ufunguo peke yake

Kila mfumo una akaunti mbili za wamiliki na nakala za kila siku, ili kazi isisimame kwa sababu ya mtu mmoja au kifaa kimoja.

Usalama kwa maneno rahisi

Kila ukurasa unafunguka kwa HTTPS, muunganisho uliofungwa. Sehemu za usimamizi zinahitaji hatua ya pili ya kuingia kutoka kwenye simu ya mhusika.

Wazi kila siku

Hali ya huduma zetu iko wazi kwa kila mtu, na ahadi yetu imeandikwa: hatuwanasi watu, tunarudisha saa.

Nataka kusoma zaidi

Watu waliofundishwa

Wanaokuhudumia wanafundishwa kwenye MOHD Academy, na vyeti vya MOHD Certified vinahakikika mtandaoni.

Nataka kusoma zaidi

Kazi yako ni ipi?

Msingi ni uleule kwa kila kazi: pesa, watu na mafunzo. Tunaanza kwa kukusikiliza, kwa maneno ya kazi yako.

Nionyeshe sekta zote 12 →

Sijaiona kazi yangu: nitawaambia ninachofanya →

Tunachotumia sisi, tunakuwekea na wewe

Wateja wako wanajibiwa usiku pia, wanakupata mtandaoni, na jina lako liko kwenye simu zao.

Nionyeshe huduma zote →

Majibu ya bure, kwa Kiswahili

Ada za shule kwa simu, madeni ya wateja, makato ya mshahara: soma leo, tumia leo.

Nataka kusoma majibu →

Timu inayojua kazi yake

Tunawafundisha watu wako, na kila mmoja anapata cheti ambacho mtu yeyote anaweza kukihakiki mtandaoni.

Nionyeshe mafunzo →

Programu zetu

Shule, duka au ofisi: chagua mlango wako

Programu tatu, akaunti moja. Ona inayokufaa kwenye mapato.africa, kwa dakika moja.

Kampuni moja, programu tatu, maisha tulivu: kila moja inaongeza nguvu kwa nyingine.

Mfumo Kamili

Milango mitatu, nyumba moja

Fedha, watu na maarifa ya shule, biashara au ofisi yako, mahali pamoja. Anza na mlango unaokufaa leo; mingine inakusubiri.

Maarifa

Kukua na Fursa

Muda wa walimu unarudi kwa watoto.

Nataka kufahamu zaidi

Mapato

Kipato na Uhuru

Pesa inayokufikia, mali unayoweza kuuza au kurithisha, na uhuru wa wakati wako.

Nataka kufahamu zaidi

Maslahi

Uhakika na Mshikamano

Siku ya mshahara bila presha.

Nataka kufahamu zaidi
  • Leo: akaunti moja tayari inafungua Maarifa, Mapato na Maslahi.
  • Andika mara moja tu. Mshahara ukilipwa, vitabu vinajiandika vyenyewe.Inakuja

Kwa nini tupo?

Watu hawatafuti pesa tu; wanatafuta uhuru. Shule, biashara au ofisi ikimeza muda, usingizi na amani ya mwenyewe, kitu kimeharibika.

Tupo ili urudi kuwa mwenye kazi yako, si mtumwa wake, na ujenge kitu cha kurithisha.

“Kutoka uwezo hadi urithi.”

Uongozi na Mawasiliano

Mfahamu Mwanzilishi mwenza

Mohd Asaa Khamis
Mohd Asaa Khamis
Mwanzilishi mwenza, na mtaalamu wa mabadiliko ya kidijitali

Anaamini kila mwenye shule, biashara au ofisi anastahili kupata muda wake tena.

Ujumbe wa Mwanzilishi mwenza · mfululizo wa sehemu tatuSehemu tatu: Utajiri, Uamuzi, Umakini.Sehemu ya 1 · UtajiriSoma →Sehemu ya 2 · UamuziSoma →Sehemu ya 3 · UmakiniSoma →

Kuanzia 01/01/2027 malipo yaliyotajwa kisheria lazima yawe ya kielektroniki. Je, biashara yako iko tayari?

Nipime utayari wangu →

Maswali 8. Taarifa ya jumla, si ushauri wa kisheria.

Unajua unachotaka kujenga. Tuanze na kinachokuuma leo.

Tunajibu kwa Kiswahili, Kiingereza au Kiarabu.